Kwa mujibu wa shirika la habari la Abna, gazeti la Kiyahudi «Haaretz» katika ripoti yake lilikiri kwamba «enzi ya utawala wa Marekani na ulimwengu wa nguvu moja, na kwa sababu hiyo enzi ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa sasa wa Israel, imekwisha.»
Katika muendelezo wa ripoti ya Haaretz imesema: «Lengo la vita lilikuwa kumzuia Iran, lakini vita viliisha huku Iran ikikaribia hadhi ya nchi ya kwanza yenye nguvu katika eneo la Ghuba ya Uajemi zaidi ya wakati wowote.»
Gazeti hili la Kizayuni hivi karibuni pia liliandika katika ripoti: «Trump alisema kwamba atafungua Mlango wa Hormuz, lakini ikabainika kwamba ndio Iran inayoendesha mchezo.»
Maoni yako